Matangazo ya Usharika tarehe 16 Machi 2025

MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 16 MACHI, 2025  

SIKU YA BWANA YA 5 KABLA YA PASAKA  

NENO LINALOTUONGOZA NI  

TUPINGE UKATILI KWA NENO LA MUNGU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 09/03/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

TANGAZO: Mkutano Mkuu wa Usharika Azania Front Cathedral

Washarika wote mliojiandikisha, mnakaribishwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Usharika wa Azania Front Cathedral utakaofanyika siku ya Jumapili tarehe 30/3/2025 usharikani Azania Front. Mkutano huo utaanza mara tu baada ya ibada kukamilika.

Siku hiyo, ibada itakuwa moja na itaanza saa 02:00 asubuhi.

Bwana akuwezeshe kuhudhuria!

--------------------------------------------------

Imetolewa: 15/3/2025

Siku ya Wanawake Duniani: Washarika Waaswa Kufanya Maombi Kushinda Majaribu

Siku ya Jumapili, Machi 9, 2025 ilifanyika ibada ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front. Ibada za aina hii hufanyika kila Jumapili ya kwanza ya mwezi Machi kila mwaka ili kutoa fursa kwa wanawake kuongoza matukio na huduma zote za ibada. 

Akizungumza katika ibada hiyo, Mama Anna Mzinga (mhubiri wa siku), aliwapongeza wanawake na washarika wote kwa kufanikisha kufanyika kwa ibada hizo. Mama Mzinga alisoma neno la siku kutoka katika kitabu cha Luka 22: 40 – 46; Somo: Mungu Hutuwezesha Kushinda Majaribu.