Matangazo ya Usharika tarehe 23 Juni 2024

MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 23 JUNI, 2024

SIKU YA BWANA YA 4 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA NI

IWENI NA HURUMA 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia kwa cheti. ili tuwakaribishe.

3. Matoleo ya Tarehe 16/06/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

TANGAZO: Kambi ya Watoto Kufanyika AZF Cathedral Tarehe 27-28 Juni 2024

Kambi ya Watoto itafanyika siku za Alhamisi na Ijumaa (Trh 27-28 Juni 2024) katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front. Muda wa semina ni kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 10 jioni.

Wazazi na walezi mnaombwa kuwaruhusu au kuwaleta watoto ili waweze kushiriki kikamilifu katika semina hii MUHIMU ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuwajenga watoto kwenye masuala ya kiafya pamoja na kiimani.

Watoto wote wa Shule ya Jumapili (Sunday School) pamoja na wale wanaoendelea na waliohitimu kipaimara mwaka jana wanakaribishwa.

MUHIMU: Zingatia muda wa semina!