Event Date: 
24-06-2024

Kambi ya Watoto itafanyika siku za Alhamisi na Ijumaa (Trh 27-28 Juni 2024) katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front. Muda wa semina ni kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 10 jioni.

Wazazi na walezi mnaombwa kuwaruhusu au kuwaleta watoto ili waweze kushiriki kikamilifu katika semina hii MUHIMU ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuwajenga watoto kwenye masuala ya kiafya pamoja na kiimani.

Watoto wote wa Shule ya Jumapili (Sunday School) pamoja na wale wanaoendelea na waliohitimu kipaimara mwaka jana wanakaribishwa.

MUHIMU: Zingatia muda wa semina!

Imetolewa na Uongozi wa Usharika; Azania Front Cathedral.