Date: 
28-06-2024
Reading: 
Luka 9:37-42

Ijumaa asubuhi tarehe 28.06.2024

Luka 9:37-43

37 Ikawa siku ya pili yake, waliposhuka mlimani, mkutano mkubwa ulikutana naye.

38 Na tazama, mtu mmoja katika mkutano alipaza sauti, akisema, Mwalimu, nakuomba umwangalie mwanangu; kwa kuwa yeye ni mwanangu pekee.

39 Na tazama, pepo humpagaa, naye mara hupiga kelele; tena humtia kifafa, huku anatokwa na povu, wala hamwachi ila kwa shida, akimchubua-chubua.

40 Nikawasihi wanafunzi wako wamtoe, wasiweze.

41 Yesu akajibu akasema, Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka, nitakaa nanyi na kuwachukulia hata lini? Mlete mwanao hapa.

42 Alipokuwa katika kumwendea, pepo akambwaga chini, akamtia kifafa. Yesu akamkemea pepo mchafu, akamponya mtoto, akamrudishia babaye.

43 Wote wakashangaa, wakiuona ukuu wa Mungu. Nao walipokuwa wakiyastaajabia mambo yote aliyoyafanya, aliwaambia wanafunzi wake,

Iweni na huruma;

Tunamsoma ndugu aliyemjia Yesu akiomba amponye mtoto wake wa pekee aliyekuwa akiugua kifafa. Ndugu huyu anakiri kuwa aliwahi kumpeleka mtoto wake kwa wanafunzi wa Yesu lakini walishindwa kuomba mtoto yule apone. Tunaona Yesu akikemea pepo, na mtoto anapona kifafa na Utukufu wake (Kristo) unadhihirika.

Tumeona wanafunzi wakishindwa kutoa pepo. Hawakuwa na imani au walikosa huruma? Au vyote? Tunalo la kujifunza hapa, kwamba katika imani yetu, tuwe na huruma.

Lakini funzo muhimu zaidi, ni huruma ya Yesu kwa mtoto aliyeponywa. Yesu mwenye huruma anatuita kurudi kwake, lakini nasi tukiwa na huruma kwa wenzetu kama Kristo mwenyewe. Huruma hutuweka pamoja. Amina

Ijumaa njema 

Heri Buberwa