Date: 
17-06-2024
Reading: 
Waefeso 4:5-7

Jumatatu asubuhi tarehe 17.06.2024

Waefeso 4:5-7

5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.

6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.

7 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.

Umoja wetu, nguvu yetu;

Mtume Paulo anawaandikia watu wa Efeso kuenenda kama wanavyoustahili wito wao waliotiwa katika Kristo. Anawaita kuwa wanyenyekevu, wapole, wavumilivu, wakichukuliana katika upendo. Anawakumbusha kuwa wameitwa na Bwana mmoja, kwa imani moja na ubatizo mmoja.

Mstari wa sita unataja kwamba Mungu aliyewaita ni Mungu mmoja aliye Baba wa wote, aliye juu ya vyote.

Kumbe kwa imani moja tumeitwa na Mungu mmoja, ndiyo maana tunaishi pamoja na tunaabudu pamoja. Basi tudumu katika kufanya yote kwa pamoja, kwa Utukufu wa Mungu ili kuutangaza Ufalme wake. Amina

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com