MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 13 JULAI, 2025

SIKU YA BWANA YA 4 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA NI

KIJANA MKRISTO NI CHACHU YA MAENDELEO

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 06/07/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 06/07/2025 ni Washarika 882. Sunday School 170

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Leo jumapili tarehe 13/7/2025 ni sikukuu ya Vijana. Hivyo ibada zote zitaongozwa na vijana.  

8. Tarehe 27/9/25 na 28/9/25 itakuwa ni sikukuu ya Mikaeli na Watoto. Hivyo tunaomba vikundi vyote vizingatie sherehe hii muhimu, ili tuweze kuwaenzi, kuwatunza na kuwatia moyo watoto wetu kwa kuwachangia chochote ili kufanikisha sikukuu hii. Mungu awabariki sana.

9. Jumamosi ya tarehe 09.08.2025 kutakuwa na ibada maalumu ya wazee wetu kuanzia miaka 65 na kuendelea, ibada hii itakayofanyika hapa Usharikani kuanzia saa 3.00 asubuhi ikiambatana na Chakula cha Bwana. Pia baada ya ibada hiyo kutakuwa na mazungumzo. Washarika tuendelee kuiombea ibada.

10.  Jumapili ijayo tarehe 20/07/2025 tutatembelewa na wageni Kwaya Kuu kutoka Usharika Kinondoni jimbo la Kaskazini. Washarika tuwaombee.

11. NDOA: 

Hakuna ndoa za washarika. 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na duka letu la vitabu.

12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mzee Evatt Kuzilwa
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mathew Munisi
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Familia ya Allen David
  • Kinondoni: Kwa ………………….. 
  • Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi Hillary Towo
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
  • Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Allen Kaduri

13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili watashirikiana na vijana.  

 Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.