MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 10 AGOSTI, 2025
SIKU YA BWANA YA 8 BAADA YA UTATU
 
NENO LINALOTUONGOZA NI
UCHAGUZI WA BUSARA
 
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
 
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
 
3. Matoleo ya Tarehe 03/08/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
 
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 03/08/2025 ni Washarika 640 Sunday School 243, Ibada ya Wazee 104
 
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
 
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
 
7. Jana Jumamosi tarehe 09.08.2025 kulikuwa na ibada maalumu ya wazee wetu kuanzia miaka 65 na kuendelea, ibada hii ilifanyika hapa Usharikani kuanzia saa 3.00 asubuhi ikiambatana na Chakula cha Bwana pamoja na mazungumzo. Tunamshukuru Mungu kwa ibada hii nzuri sana.
 
8. Chaplain wetu anaomba kukutana na vikundi vyote vya Kwaya hapa Usharikani jumanne ijayo tarehe 12/08/2025 saa 11.00 jioni. Vikundi vyote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa na kufika kwa Wakati.
 
9. Uongozi wa shule ya jumapili unapenda kuwaomba wazazi na walezi kuwahimiza watoto siku ya jumamosi ijayo tarehe 16/08/2025 kufika kufanya mtihani wa shule ya jumapili ili kupata washindi watakaowakilisha Jimboni. Mungu awabariki sana.
 
10. Uongozi wa vijana Azania unapenda kuwashukuru vijana wote walioshiriki kwenye mechi ya jumapili iliyopita, mchezo ulikuwa mzuri na tuliweza kutoka droo, hivyo tunaendelea na round ya pili leo jumapili tarehe 10/8/25 kati ya usharika wa Azania na Usharika wa Tabata. Vijana na washarika wote tunakaribishwa kwenda kuangalia mechi hii ya leo. Mungu awabariki.
 
11. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA KWANZA TUNANGAZA NDOA YA TAREHE 30/08/2025
SAA 9.00 ALASIRI
  •  Bw. Stuart Gamaliel Kisyombe na Bi. Paschalina Marijani Msofe

 
12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
 
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo:
Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo.
 
- Upanga: Kwa Mama Gembe
 
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa ………………………..
 
- Kinondoni: Kwa Prof. Geofrey Mmari
 
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa
…………………………………………..
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
 
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Mchungaji na Mama Charles Mzinga
 
13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front.org pia tupo Facebook na Instagram.
 
14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili.
 
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.