MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 20 JULAI, 2025
SIKU YA BWANA YA 5 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA NI
TUDUMU KATIKA FUNDISHO LA KRISTO
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 13/07/2025
Jumla - Tshs 20,060,000/= USD 26/=
MATOLEO KATIKATI YA WIKI
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 13/07/2025 ni Washarika 720. Sunday School 209
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Jumapili ijayo tarehe 27/7/2025 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.
8. Tarehe 27/9/25 na 28/9/25 itakuwa ni sikukuu ya Mikaeli na Watoto. Hivyo tunaomba vikundi vyote vizingatie sherehe hii muhimu, ili tuweze kuwaenzi, kuwatunza na kuwatia moyo watoto wetu kwa kuwachangia chochote ili kufanikisha sikukuu hii. Mungu awabariki sana.
9. Jumamosi ya tarehe 09.08.2025 kutakuwa na ibada maalumu ya wazee wetu kuanzia miaka 65 na kuendelea, ibada hii itakayofanyika hapa Usharikani kuanzia saa 3.00 asubuhi ikiambatana na Chakula cha Bwana. Pia baada ya ibada hiyo kutakuwa na mazungumzo. Tunawakaribisha wazee kutoa maoni yao kuandaa siku hiyo. Washarika tuendelee kuiombea ibada hiyo.
10 Leo tarehe 20/07/2025 tumetembelewa na wageni Kwaya Kuu kutoka Usharika Kinondoni jimbo la Kaskazini.
11. Uongozi wa Umoja wa wanawake Azania Front una furaha kuwatangazia kuwa jumapili ijayo tarehe 27.7.2025 wanawake mtaa wetu wa Tabora wataleta mbogamboga na vitu vingine vya shambani walivyovuna mashambani kwao, vitu hivyo vitauzwa baada ya ibada zote hapo nje. Washarika tujiandae kununua mazao fresh kutoka shambani. Karibuni wote
12. NDOA: Ndoa za washarika.
KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 08/08/2025
SAA 6.00 MCHANA
-
Bw. Nicholas Kerya Kisiri na Bi. Irene Adolph Kinyanguli
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na duka letu la vitabu.
13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mzee Evatt Kuzilwa
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi George Kinyaha
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Nyamajeje Buchanagandi
- Kinondoni: Kwa …………………..
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana Dudley Mawala
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Kelvin Matandiko
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Robinson Monyo.
14. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
15. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
NENO: Zab. 2:6-8Mt. 5:17-191Tim. 4:13-16