Chaplain Charles Mzinga Aongoza Ziara Mtaa wa Tabora

Jumapili ya tarehe 17 Septemba 2023, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral, Chaplain Charles Mzinga aliongoza ujumbe wa Usharika kwenye ziara iliyofanyika mtaa wa Tabora, miongoni mwa mitaa inayotunzwa na Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral.

Akiwa mtaani hapo, Chaplain Mzinga aliongoza ibada takatifu iliyohudhuriwa na washarika wa mtaa huo. Katika ibada hiyo, jumla ya watoto wadogo saba (7) walibatizwa na washarika walipata fursa ya kushiriki Meza ya Bwana.