Date: 
22-09-2023
Reading: 
Mathayo 15:29-31

Ijumaa asubuhi tarehe 22.09.2023

Mathayo 15:29-31

29 Yesu akaondoka huko, akafika kando ya bahari ya Galilaya; akapanda mlimani, akaketi huko.

30 Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya;

31 hata ule mkutano wakastaajabu, walipowaona mabubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Mungu hujishughulisha na maisha yetu;

Yesu akiwa katika huduma yake, alifika kando ya bahari ya Galilaya, akapanda mlimani na kuketi huko. Kule makutano walimletea wagonjwa na wenye shida mbali mbali akawaponya. Viwete, bubu, vilema, vipofu na wengine wengi waliponywa na Yesu. Kilichotokea kwa makutano ni kustaajabu, na kumtukuza Mungu. 

Somo linaonesha Yesu akiponya wagonjwa walioletwa kwake na makutano waliomfuata. Yesu alihubiri, alifundisha na kuponya. Alijishughulisha na maisha ya watu wake. Hata leo hufanya vivyo hivyo, akituita kumwamini na kumfuata daima. Mwamini Yesu uokolewe. Amina.

Ijumaa njema.

Heri Buberwa