Date: 
19-09-2023
Reading: 
Yohana 9:6-12

Jumanne asubuhi 19.09.2023

Yohana 9:6-12

6 Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho,

7 akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona.

8 Basi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji, wakasema, Je! Huyu siye yule aliyekuwa akiketi na kuomba?

9 Wengine wakasema, Ndiye. Wengine wakasema, La, lakini amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye.

10 Basi wakamwambia, Macho yako yalifumbuliwaje?

11 Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona.

12 Wakamwambia, Yuko wapi huyo? Akasema, Mimi sijui.

Mungu hujishughulisha na maisha yetu;

Yesu alimwona mtu kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamuuliza, kwa yule kipofu nani alitenda dhambi, yule kipofu au wazazi wake? Yesu akawajibu akisema kuwa hakuna aliyetenda dhambi, bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. 

Ndipo tunasoma Yesu akitema mate chini na kufanya tope, akampaka yule kipofu na kumuelekeza akanawe kwenye birika la Siloamu, akarudi anaona. Huyu ndugu aliyekuwa kipofu alishuhudia jambo hili kwa nguvu zote.

Ilikuwa tabia ya Yesu kujali maisha ya watu. Ndiyo maana hakumuacha huyu ndugu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Alijishughulisha na maisha yake. Hata leo Yesu hujishughulisha na maisha yetu, akituita kumwamini na kumfuata yeye daima. Tudumu katika yeye siku zote, ili tuwe na mwisho mwema. Amina.

Jumanne njema.

 

Heri Buberwa