23 Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng'ombe zako.
24 Kwa maana mali haziwi za milele; Na taji je! Yadumu tangu kizazi hata kizazi?
25 Manyasi huchukuliwa, na majani mabichi huonekana, Na maboga ya milimani hukusanyika.
26 Wana-kondoo hufaa kwa mavazi yako; Na mbuzi ni thamani ya shamba
27 Tena yatakuwapo maziwa ya mbuzi, Ya kukutosha kwa chakula chako, Na chakula cha watu wa nyumbani mwako, Na posho la vijakazi vyako.
Uwakili wetu kwa Bwana;
Mwandishi anaelekeza kufanya bidii katika kujua makundi ya wanyama na mali zote kwa ujumla. Pamoja na hilo, anaeleza kwamba mali huwa hazidumu milele. Mali zote ikiwemo fedha, wanyama, nyumba na nyinginezo zote hutoweka. Msingi wa hoja ya mwandishi ni kwa aaminiye kufahamu nafasi yake katika mali, akijua kuwa mali hizo hutoweka lakini mwisho wetu ni katika Bwana.
Kama tulivyosoma, tunapoweka bidii kujua nafasi ya mali tulizopewa, bidii hiyo itufanye kufahamu kuwa mali tulizo nazo siyo zetu, bali za Bwana. Sisi tumewekwa tu kuwa mawakili, tutunze kwa uaminifu. Tukijua nafasi yetu kama mawakili wa Bwana, tutimize wajibu huo kwa uaminifu maana tutatoa hesabu. Amina.
Alhamisi njema!
----------------------------------------
Heri Buberwa
Mlutheri