Date: 
26-06-2024
Reading: 
Waefeso 4:32

Jumatano asubuhi tarehe 26.06.2024

Waefeso 4:32

Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

Iweni na huruma;

Mtume Paulo anawaandikia Waefeso kuwa wafadhili wao kwa wao. Hapa anawapa ujumbe wa kusaidiana katika maisha ya kila siku. Anaendelea kuwaambia kuwa wawe wenye huruma na kusameheana wao kwa wao. Hapa aliwataka kila mmoja kumuona mwenzie wa thamani, hivyo wote kukaa pamoja kama Kanisa la Kristo.

Kusaidiana kupo miongoni mwetu?

Tunaonena huruma?

Tunasameheana?

Tunaalikwa kuishi kama kundi la waaminio, kila mmoja akimuona mwenzake kama mtu wa thamani maana kwa umoja wetu sisi ni mwili wa Kristo. Amina

Jumatano njema 

Heri Buberwa