DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 28 SEPTEMBA, 2025
SIKUKUU YA WATOTO: MIKAELI NA MALAIKA WOTE
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
TUWAPENDE NA KUWAJALI WATOTO KATIKA BWANA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 21/09/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 21/09/2025 ni Washarika 672 Sunday School 264
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Leo jumapili tarehe 28/09/2025 ni sikukuu ya Mikaeli na watoto. Hivyo ibada zote zinaongozwa na watoto wakishirikiana na wazee kundi la Kwanza.
8. Umoja wa Vijana Azania Front unapenda kuwataarifu kwa furaha kuwa Idara ya Ustawi wa Kijana imeandaa SEMINA MTANDAONI YA KIMKAKATI NA YA MAFUNZO MAZURI tarehe 02 Oktoba kuanzia saa mbili usiku. Kichwa cha Semina: "Kijana na Uhusiano wake na Mungu.” Kwa maelezo zaidi onana na viongozi wa Umoja wa vijana.
9. Jumapili ijayo tarehe 05/10/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.
10. Uongozi wa Umoja wa Wanaume unatangaza Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wanaume utakaofanyika hapa kanisani siku ya Jumapili tarehe 19/10/2025 mara baada ya Ibada ya tatu. Wanaume wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa. Wanaume wote wa Usharika huu wenye mapenzi mema na Jukwaa ambao hawajajiunga wanakaribishwa kujiunga na wenzao. Kutakuwa na viburudisho pamoja na virutubisho kwa ajili ya afya za washiriki.
11. Jumapili ya tarehe 26/10/2025 ni sikukuu ya mavuno. Ibada itakuwa ni moja itakayoanza saa 2.00 asubuhi. Hivyo washarika tujiandae vizuri na tuendelee kuiombea siku hiyo muhimu.
12. NDOA: HAKUNA NDOA ZA WASHARIKA
Lakini matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mbwilo
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa ……………………
- Kinondoni: Kwa ………………………….
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay, Masaki: Kwa Mama Nisile Mollel
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bw & Bibi Itemba
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Prof. William Matuja
14. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
15. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza wakishirikiana na watoto.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.