Date: 
22-06-2024
Reading: 
Wafilipi 1:27-30

Jumamosi asubuhi tarehe 22.06.2024

Wafilipi 1:27-30

27 Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;

28 wala hamwogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara mathubuti ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokovu, huo utokao kwa Mungu.

29 Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake;

30 mkiwa na mashindano yale yale mliyoyaona kwangu, na kusikia kwamba ninayo hata sasa.

Umoja wetu, nguvu yetu;

Mtume Paulo anawaandikia watu wa Ufilipi kuwa mwenendo wao uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, yaani wasimame imara katika Injili. Katika kusimama huko anawahakikishia kutowaogopa adui zao kwa neno lolote maana kwa umoja wao wanayo nguvu ya wokovu utokao kwa Mungu.

Ukiangalia ujumbe wa Mtume Paulo ni msisitizo wa kukaa pamoja katika maisha ya imani ili kazi ya kuhubiri Injili iendelee. Ndiyo maana anawaambia kwa pamoja wawe na mwenendo mwema katika Kristo ili wawe imara. Nasi tunakumbushwa kuwa na mwenendo mwema kwa umoja wetu, ili Kristo atukuzwe daima, na watu wote waokolewe kwa sisi kumhubiri yeye. Amina.

Jumamosi njema 

Heri Buberwa