Date: 
24-06-2024
Reading: 
Luka 14:1-6

Jumatatu asubuhi tarehe 24.06.2024

Luka 14:1-6

1 Ikawa alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia.

2 Na tazama, mbele yake palikuwa na mtu mwenye ugonjwa wa safura.

3 Yesu akajibu, akawaambia wana-sheria na Mafarisayo, Je! Ni halali kuponya siku ya sabato, ama sivyo?

4 Wao wakanyamaza. Akamshika, akamponya, akamruhusu aende zake.

5 Akawaambia, Ni nani miongoni mwenu, ikiwa ng'ombe wake au punda wake ametumbukia kisimani, asiyemwopoa mara hiyo siku ya sabato?

6 Nao hawakuweza kujibu maneno haya.

Iweni na huruma;

Yesu aliingia kwenye nyumba ya Farisayo mmoja siku ya sabato kula chakula. Mara mbele yake kulikuwa na mgonjwa wa safura, akamponya. Mafarisayo hawakuamini katika kazi yoyote ikiwapo uponyaji katika siku ya sababo, lakini Yesu alipowauliza kama ni sahihi kuponya siku ya sababo au hapana, walinyamaza. 

Yesu aliendela kuwauliza, kuwa ikitokea ng'ombe au punda ametumbukia kisimani wangemuacha kwa sababu ni sabato? Wakanyamaza! Mafarisayo walizingatia sheria, na siyo neema ya Mungu. Kristo alileta neema, na kwa neema hii alimponya mgonjwa wa safura aliyemkuta nyumbani kwa Farisayo. Mwamini Yesu uokolewe. Amina.

Uwe na wiki njema

 

Heri Buberwa