Hii ni Kwaresma
Jumatano asubuhi tarehe 19.03.2025
Mathayo 2:13-16
13 Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.
14 Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri;
15 akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nalimwita mwanangu.
16 Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi.
Tupinge ukatili kwa neno la Mungu;
Baada ya Mamajusi kumuona na kumsujudia mtoto Yesu, wanaelekezwa na malaika wasirudi kwa Herode, wakarudi kwa njia nyingine, maana Herode alipanga kumuua mtoto. Ndipo katika somo la leo asubuhi, malaika anamtokea Yusufu akimwambia kumpeleka mtoto Yesu Misri, ili asiuawe na Herode. Lakini bado Herode aliendelea na ukatili, akawaua watoto wote wadogo, akilenga kumuua Yesu!
Tupo miongoni mwetu leo wenye roho kama ya Herode? Katili, tulio tayari hata kuua kwa sababu ya maslahi binafsi? Hii haitakiwi kabisa, maana mwenye hii tabia hataiepuka ghadhabu ya Mungu. Upendo wa Mungu utawale miongoni mwetu kwa ajili ya Utukufu wake, tusiwe na roho mbaya, maana ukatili ni uovu.
Jumatano njema
Heri Buberwa