MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 16 MACHI, 2025
SIKU YA BWANA YA 5 KABLA YA PASAKA
NENO LINALOTUONGOZA NI
TUPINGE UKATILI KWA NENO LA MUNGU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 09/03/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 09/03/2025 ilikuwa ni washarika 773. Sunday School 181
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Jumapili ijayo tarehe 23/03/3025 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.
7. Uongozi wa shule ya jumapili unapenda kuwatangazia wazazi kuwa jumapili ya tarehe 23/03/2025 ni siku ya maombi ya dunia kwa watoto wa shule ya jumapili. Hivyo watoto wachache wataongoza maombi kwenye ibada ya wakubwa wakiwakilisha wenzao. Na siku hiyo watatoa sadaka ambayo watakwenda nayo Mtoni kwa watoto wenye utindio wa ubongo tarehe 29/03/2025.
8. Jumapili ya Tarehe 30/03/2025 tutakuwa na Mkutano Mkuu wa Usharika. Hivyo ibada itakuwa ni moja tu itakayoanza saa 2.00 asubuhi. Washarika tuendelee kuombea mkutano huo muhimu.
9. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
10. Tunaendelea na ibada za Kwaresma kila siku ya jumatano saa 11.00 jioni. Kwaya zote zitahudumu. Zamu za wazee itakuwa ni kundi la Kwanza
11. Tunapenda kuwataarifu washarika wanaohitaji huduma ya Youtube live Streaming, Video, Still Pictures na Matarumbeta zinapatikana kwa matukio yote yanayofanyika hapa Usharikani. Kwa maelezo zaidi na gharama fika ofisi ya Mhasibu.
12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Eng & Dr Matee
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mathew Munisi
- Kawe,Mikocheni , Mbezi Beach Watasali katika ibada ya kwaresma kanisani
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Lawrence Mlaki
- Oysterbay/Masaki: Watasali katika ibada ya kwaresma kanisani Kinondoni: Kwa …………………………………
- Mjini kati: Watafanyia hapa kanisani saa 1.00 asubuhi.
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa ……………………………………..
13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front.org, pia tupo Facebook na Instagram.
14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.