Date: 
26-03-2025
Reading: 
Matendo 9:32-34

Hii ni Kwaresma 

Jumatano asubuhi tarehe 26.03.2025

Matendo ya Mitume 9:32-34

32 Hata Petro alipokuwa akizunguka-zunguka pande zote akawatelemkia na watakatifu waliokaa Lida.

33 Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea, mtu huyo amelala kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza.

34 Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya; ondoka, ujitandikie. Mara akaondoka.

Tumtazame Bwana aliye tumaini;

Petro anaendelea na utume wake anafika Lida na huko anamkuta ndugu mmoja aliyeitwa Ainea. Huyu alikuwa amelala kitandani kwa miaka minne, na mstari wa 33 unasema alikuwa amepooza. Haiandikwi kama mgonjwa huyu aliomba lolote, au ndugu yeyote labda aliyemuuguza, kinachoonekana ni Petro kumwombea uponyaji kwa njia ya Yesu Kristo.

Mgonjwa aliyekuwa amepooza na kulala kitandani kwa miaka minne anapona kwa jina la Yesu. Huenda mgonjwa huyu alikuwa amepata tiba kadhaa? Na maombi kadhaa? Lakini Petro alipoomba uponyaji akapona, kwa njia ya Yesu Kristo. Kumbe tukimtazama Yesu anatuwezesha katika yote. Basi tumtazame Yesu Kristo aliye tumaini letu. Amina

Jumatano njema 

Heri Buberwa