MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 30 MACHI, 2025  

SIKU YA BWANA YA 3 KABLA YA PASAKA  

NENO LINALOTUONGOZA NI  

TUTUNZE UUMBAJI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 23/03/202Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 23/03/2025 ilikuwa ni washarika 794. Sunday School 119

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Jumapili ijayo tarehe 06/04/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae

7. Uongozi wa umoja wa wanawake unapenda kuwaomba wanawake wote kuungana na wanawake Jimbo la kati kwenye maadhimisho ya Pasaka yatakayofanyika tarehe 12/04/2025 Usharika wa Mabibo External ngazi ya Jimbo.

8. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

9. Tunaendelea na ibada za Kwaresma kila siku ya jumatano saa 11.00 jioni. Kwaya zote zitahudumu. Wazee wote watakuwa zamu.

10. Tunapenda kuwataarifu washarika wanaohitaji huduma ya Youtube live Streaming, Video, Still Pictures na Matarumbeta zinapatikana kwa matukio yote yanayofanyika hapa Usharikani. Kwa maelezo zaidi na gharama fika ofisi ya Mhasibu. 

11. Wiki hii tutakuwa na Kipindi maalum cha kujifunza Neno la Mungu na kuomba ambacho kitafanyika siku ya Alhamisi na Ijumaa kuanzia saa 11.00 jioni. Fursa hii imewekwa Maalum ili kupata muda wa kutosha wa tafakari na maombi, tukikumbuka tendo Kuu la Mungu kuturejeshea tena nafasi ya kuwa utukufu wa urithi wake kwa kufa na kufufuka kwake Yesu. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral. Wote mnakaribishwa!

12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Ruth Korosso
  • Upanga: Kwa Mama Teri
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Francis Mwaitembo
  • Mjini kati: Watafanyia hapa kanisani saa 1.00 asubuhi.
  • Oysterbay/Masaki: Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kawe,Mikocheni , Mbezi Beach Watasali katika ibada ya kwaresma kanisani  

13.  Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front.org, pia tupo Facebook na Instagram.

14.  Zamu: Zamu za wazee ni Wazee wote watakuwa zamu  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.