Date: 
18-03-2025
Reading: 
2 Mambo ya nyakati 13:23-27

Hii ni Kwaresma 

Jumanne asubuhi tarehe 18.03.2025

2 Mambo ya Nyakati 18:23-27

23 Ndipo akakaribia Zedekia mwana wa Kenaana, akampiga Mikaya kofi la shavu, akasema, Alitokaje kwangu roho ya Bwana ili aseme na wewe?

24 Mikaya akasema, Angalia utaona siku ile, utakapoingia katika chumba cha ndani ili ujifiche.

25 Mfalme wa Israeli akasema, Mchukueni Mikaya mkamrudishe kwa Amoni mkuu wa mji, na kwa Yoashi mwana wa mfalme;

26 mkaseme, Mfalme asema hivi, Mtieni huyu gerezani, mkamlishe chakula cha shida, na maji ya shida, hata nitakaporudi kwa amani.

27 Mikaya akasema, Ukirudi kabisa kwa amani, Bwana hakusema kwa mimi. Akasema, Sikieni, enyi watu wote.

Tupinge ukatili kwa Neno la Mungu;

Sura ya 18 ya Mambo ya Nyakati hueleza juu ya Mfalme Yehoshafati wa Yuda aliyeungana na Mfalme Ahabu wa Israeli kuipiga Ashuru, hadi kusababisha kufa kwa Ahabu, na kudhoofika kwa Yehoshafati, baada ya Nabii Mikaya kuwa ametabiri maafa husika. Hata baada ya Mikaya kutoa unabii wa Israeli kutofanikiwa katika vita, Mfalme Yehoshafati bado aliendelea na mpango wake! Pamoja na Yehoshafati kunusurika kifo, kuungana kwake na Ahabu lilikuwa kosa kubwa! 

Jumapili iliyopita tuliona Yeremia akitoa unabii kuhusu kuharibiwa kwa Yerusalemu, unabii ambao ulikataliwa na makuhani na manabii. Ni kama leo asubuhi, Yehoshafati anaacha kuupokea unabii wa Mikaya kwamba shambulizi lake kwa Ashuru lisingefanikiwa! Kusikiliza ni vizuri, maana husaidia kuamua vema na kutuepusha na matendo maovu. Amina

Jumanne njema

 

Heri Buberwa