Date: 
31-03-2025
Reading: 
Mhubiri 11:8

Hii ni Kwaresma 

Jumatatu asubuhi tarehe 31.03.2025

Mhubiri 11:6

Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiuzuie mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa,kama ni hii au hii,au kama zote zitafaa sawasawa.

Tutunze uumbaji (mazingira)

Sura ya kumi na moja ya kitabu cha mhubiri huhimiza juu ya ukarimu na kuwekeza katika kazi, kwamba mafanikio ya kweli huja kwa imani na kumwamini Mungu katika bidii ya kazi. Hata pale inapotokea matokeo yakawa kinyume na mategemeo, msisitizo ni kukaa katika Bwana mwenye hatma ya wote wamchao. Sura hii inatumia uoto wa asili kusisitiza kazi, kwa maana ya kutunza uasili wa Mungu kwa maana ya uumbaji.

Kipekee kwa somo la leo asubuhi, mstari wa sita unaelekeza kupanda mbegu asubuhi na jioni, kuonesha kwamba tunatakiwa kuwa makini, kuwa na bidii pia katika kazi, na siyo kuwa wavivu. Kumbe tunakumbushwa kuwa tunaishi katika dunia ambayo ni uumbaji wa Mungu, ambamo pamoja na kazi zetu, kuitunza dunia hii ni wajibu wetu. Kupanda mbegu leo tunaweza kusema ni kufanya kazi. Kumbe katika kufanya kazi zetu, tutunze uumbaji wa Mungu. Amina

Uwe na wiki njema

Heri Buberwa