Kwaya ya Agape yafariji Watoto Muhimbili Hosp.

Hivi karibuni Kwaya ya Agape inayohudumu katika ibada ya Kiswahili, kila Jumapili saa moja asubuhi katika Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront Cathedral waliwatembelea watoto wenye mahitaji mbalimbali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuwapa mkono wa faraja.

Watoto walionufaika na ziara hiyo ni wale wenye matatizo ya ugonjwa wa mgongo wazi na wale wenye matatizo ya vichwa vikubwa. Ziara ya kuwatembelea watoto hao ilifanyika tarehe 14/4/2021 ambapo mbali na kupatiwa mahitaji ya siku hadi siku watoto hao pia walipata bima za afya (watoto 56).

Dayosisi ya Ziwa Victoria Wazuru Azaniafront

Siku ya Jumapili 13/05/2021 ilikuwa ni baraka kubwa kwa Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront Cathedral kuwapokea wageni, wanawake viongozi kutoka katika Dayosisi ya Ziwa Victoria. Viongozi hao wapatao sita (6) kutoka katika mitaa, sharika, na majimbo ya Dayosisi ya Ziwa Victoria waliongozwa na Mama Askofu Elifaraja Gulle, mwenza wa Askofu Gulle wa Dayosisi ya Ziwa Victoria.

Ziara ya viongozi hao wanawake katika Usharika wa Azaniafront iliambatana na msafara wa wanawake wengine 21 ambao walishiriki ibada katika mitaa na sharika mbalimbali za Dayosisi ya Mashariki na Pwani.