Date: 
21-06-2021
Reading: 
Romans 15:1-6 (Warumi)

MONDAY 21ST JUNE 2021,     MORNING                                                     

Romans 15:1-6 New International Version (NIV)

1 We who are strong ought to bear with the failings of the weak and not to please ourselves. Each of us should please our neighbors for their good, to build them up. For even Christ did not please himself but, as it is written: “The insults of those who insult you have fallen on me.”[a] For everything that was written in the past was written to teach us, so that through the endurance taught in the Scriptures and the encouragement they provide we might have hope.

May the God who gives endurance and encouragement give you the same attitude of mind toward each other that Christ Jesus had, so that with one mind and one voice you may glorify the God and Father of our Lord Jesus Christ.

God desires His people to love each other and walk in harmony. Unity asks us to give up something for the good of others. If we all are out for ourselves, there will never be unity. When we are seeking to serve others then unity and harmony are possible.


JUMATATU  TAREHE 21 JUNE 2021      ASUBUHI                                     

WARUMI 15:1-6

1 Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe.
Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe.
Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi.
Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.
Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa mfano wa Kristo Yesu;
ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Mungu anapenda watu wake wapendane na kuenenda katika umoja. Katika umoja tunaitwa kuacha jambo fulani kwa ajili ya manufaa ya wengine. Ikiwa sisi sote tutajiangalia wenyewe, kamwe hapatakuwa na umoja. Tukitafuta kuwatumikia wengine, hapo ndipo umoja na kupatana vitawezekana.