MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 08 JUNI, 2025
NENO LINALOTUONGOZA NI
ROHO MTAKATIFU NI USHINDI WETU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna Wageni waliyeotufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 01/06/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 01/06/2025 ni Washarika 736.
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Jumatatu ijayo tarehe 09/06/2025 saa 11.00 jioni kutakuwa na ibada ya kuenea kwa Roho Mtakatifu. Kwaya zote zitahudumu. Wazee wote watakuwa zamu.
7. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
8. Familia ya Bwana na Bibi Kelvin Matandiko wamepata Baraka ya mtoto wa kiume tarehe 03/06/2025 katika hospitali ya taifa Muhimbili. Baba, Mama na Mtoto wanaendelea vizuri.
9. NDOA. Ndoa za Washarika
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 14/06/2025
SAA 8.00 MCHANA
- Bw. Jimmy Witson Mushi na Bi. Joanarca Julius Caesar
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na duka letu la vitabu.
10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
- Upanga: Kwa Mama Ndossi
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Dr Abedi na Eng Elisifa Kinasha
- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale.
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa Mama Elipina Mlaki
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Dk na Bibi Henry Mwanyika.
11. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
12. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.