Date: 
28-06-2021
Reading: 
2 SAMWELI 9:1-8 (Samwel)

JUMATATU TAREHE 28 JUNI 2021, ASUBUHI

2 SAMWELI 9:1-8

1 Kisha Daudi akasema, Je! Amesalia mtu mmoja katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya Yonathani?
Palikuwa na mtumishi mmoja wa nyumba ya Sauli, jina lake Siba, basi wakamwita aende kwa Daudi; na mfalme akamwuliza, Wewe ndiwe Siba? Naye akasema Mimi, mtumwa wako ndiye.
Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu.
Mfalme akamwambia, Yuko wapi? Siba akamwambia mfalme, Tazama, yumo katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari.
Basi mfalme Daudi akatuma watu, akamwondoa katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari.
Basi Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli akaenda kwa Daudi, akaanguka kifudifudi, akasujudu. Daudi akasema, Mefiboshethi! Naye akaitika, Mimi hapa, mtumwa wako!
Daudi akamwambia, Usiogope, maana bila shaka nitakutendea mema; kwa ajili ya Yonathani, baba yako, nami nitakurudishia mashamba yote ya Sauli, baba yako; nawe utakula chakula mezani pangu daima.
Akasujudu, akasema, Mimi mtumwa wako ni nini, hata ukamwangalia mbwa mfu kama mimi?

Tunaitwa kutenda haki na Huruma.

Katika mistari ya leo hapo juu tunasoma habari ya mwana wa Yonathan, katika nyumba ya Sauli, aliyekua mlemavu wa miguu, na amedhulumiwa urithi wake. Mfalme Daudi anamtafuta na kumfariji na kumrejeshea urithi wake. Mstari  wa 8 unatuonyesha jisi kijana yule alivyokuwa amenyong’onyea hadi kujilinganisha na mbwa mfu, lakini Mfame Daudi alimwonyesha huruma na kumtendea haki.

Katika maisha yetu ya leo, tunaona mara nyingi wanyonge hawatendewi haki. Mungu atusaidie sisi sote kuwahurumia na  kuwatendea wanyonge haki.


MONDAY 28TH JUNE 2021, MORNING

1 SAMWEL 9:1-8

 1 David asked, “Is there anyone still left of the house of Saul to whom I can show kindness for Jonathan’s sake?”

Now there was a servant of Saul’s household named Ziba. They summoned him to appear before David, and the king said to him, “Are you Ziba?”

“At your service,” he replied.

The king asked, “Is there no one still alive from the house of Saul to whom I can show God’s kindness?”

Ziba answered the king, “There is still a son of Jonathan; he is lame in both feet.”

“Where is he?” the king asked.

Ziba answered, “He is at the house of Makir son of Ammiel in Lo Debar.”

So King David had him brought from Lo Debar, from the house of Makir son of Ammiel.

When Mephibosheth son of Jonathan, the son of Saul, came to David, he bowed down to pay him honor.

David said, “Mephibosheth!”

“At your service,” he replied.

“Don’t be afraid,” David said to him, “for I will surely show you kindness for the sake of your father Jonathan. I will restore to you all the land that belonged to your grandfather Saul, and you will always eat at my table.”

Mephibosheth bowed down and said, “What is your servant, that you should notice a dead dog like me?”

Read full chapter

We are called to be merciful and just.

In today's verses above we read of Jonathan's son, in the house of Saul, who was disabled in both legs, and who had been denied his inheritance. King David seeks him out, comforts him and restores his inheritance. Verse 8 shows us how young the man was lowered to be like a dead dog, but King David lifted him up, showed him mercy and justice.

In our modern life, we often see the oppressed being treated unfairly. May God help us all to be compassionate and to treat the weak with justice.