DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 13 APRILI, 2025
SIKU YA MITENDE
NENO LINALOTUONGOZA NI TUMSHANGILIE BWANA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 06/04/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 06/04/2025 ilikuwa ni washarika 603. Sunday School 242
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. RATIBA YA PASAKA
Jumamosi ijayo tarehe 19/04/2025 saa 4.00 asubuhi kutakuwa na mafundisho ya ubatizo. Wazazi na wadhamini mnaombwa kuhudhuria na kufika kwa wakati.
8. SHUKRANI - JUMAPILI IJAYO TAREHE 20 APRIL 2025
IBADA YA KWANZA SAA 1.00 ASUBUHI
- Familia ya Mwalimu Amri Hingi watamtolea Mungu shukrani kumshukuru Mungu kwa siku ya kuzaliwa kwa Mwalimu Amri Hingi na mwanae Eliah Hingi siku ya tarehe 20 April
Neno: Zaburi 23, Wimbo: Kama si wewe ( Kwaya ya Upendo)
IBADA YA TATU SAA 4.30 ASUBUHI
- Familia ya Haika Edward Sabuni watamshukuru Mungu kutimiza miaka 65 na mtoto wangu Kelvin kutimiza miaka 32 tarehe 20/04
Neno: Zaburi 146:1-
2, Wimbo: TMW 175
9. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 03/05/2025
SAA 4.00 ASUBUHI
-
Bw. Eliad Augustine Mugambila na Bi. Maryness Lwessigobuta Kilenzi
NDOA IFUATAYO ITAFUNGWA PAROKIA YA MT. THOMAS MORE – MBEZI BEACH KATI YA
-
Bw. Franklin Victor Lubuva na Bi. Doreen-Maria Dallas Mwanauta
10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
- Upanga: Watasali Ijumaa Kuu hapa Kanisani.
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bw& Bi Moses Kombe
- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki.
- Mjini kati: Kwa Bwana Peter Obama.
11. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
12. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayaba
riki.