Date: 
29-06-2021
Reading: 
2Samuel 9:9-13

TUESDAY 29TH JUNE 2021 MORNING 2 SAMUEL 9:9-13

2 Samuel 9:9-13 New International Version (NIV)

9 Then the king summoned Ziba, Saul’s steward, and said to him, “I have given your master’s grandson everything that belonged to Saul and his family. 10 You and your sons and your servants are to farm the land for him and bring in the crops, so that your master’s grandson may be provided for. And Mephibosheth, grandson of your master, will always eat at my table.” (Now Ziba had fifteen sons and twenty servants.)

11 Then Ziba said to the king, “Your servant will do whatever my lord the king commands his servant to do.” So Mephibosheth ate at David’s[a] table like one of the king’s sons.

12 Mephibosheth had a young son named Mika, and all the members of Ziba’s household were servants of Mephibosheth. 13 And Mephibosheth lived in Jerusalem, because he always ate at the king’s table; he was lame in both feet.

David had made a promise to Jonathan, his beloved friend and the son of Saul, that he would show kindness to the remaining members of Saul’s household. (See 1 Samuel 20:15-16.) David now intended to keep that promise.

Christians too have been shown God’s kindness, by grace, because of His promise to our spiritual father Abraham and His covenant through Jesus. 


JUMANNE TAREHE 29 JUNE 2021 ASUBUHI 2 SAMWELI 9:9-13

9 Ndipo mfalme akamwita Siba, mtumwa wa Sauli, akamwambia, Mali yote yaliyokuwa ya Sauli na ya nyumba yake nimempa mwana wa bwana wako.

10 Nawe utamlimia nchi hiyo, wewe, na wanao, na watumwa wako; nawe utamletea mwana wa bwana wako matunda yake, apate chakula ale; lakini Mefiboshethi, mwana wa bwana wako, atakula chakula mezani pangu sikuzote. Basi huyo Siba alikuwa na wana kumi na watano na watumwa ishirini.

11 Ndipo Siba akamwambia mfalme, Mimi, mtumwa wako, nitatenda hayo yote kama bwana wangu, mfalme, alivyoniamuru. Na kwa habari za Mefiboshethi, mfalme alisema, Atakula mezani pangu, kama mmojawapo wa wana wa mfalme.

12 Huyo Mefiboshethi alikuwa na mwana mdogo, jina lake akiitwa Mika. Na watu wote waliokaa nyumbani mwa Siba walikuwa watumwa wa Mefiboshethi.

13 Basi Mefiboshethi akakaa Yerusalemu; maana alikuwa akila chakula sikuzote mezani pa mfalme; naye alikuwa na kilema cha miguu yote miwili.

Daudi alimuahidi Yonathani, rafiki yake mpendwa aliyekuwa mtoto wa Sauli, kwamba angetenda wema kwa watu waliosalia katika nyumba ya Mfalme Sauli (1 Samuel 20:15-16). Sasa Mfalme Daudi aliazimia kutimiza ahadi hiyo. 

Wakristo pia tumetendewa wema wa Mungu, kwa neema, kwa sababu ya ahadi yake kwa baba yetu wa kiroho Ibrahimu na agano lake kwa njia ya Yesu Kristo.