Date: 
16-06-2021
Reading: 
Acts 17:24-29 (Matendo)

WEDNESDAY 16TH JUNE 2021   MORNING                                     

Acts 17:24-29 New International Version (NIV)

24 “The God who made the world and everything in it is the Lord of heaven and earth and does not live in temples built by human hands. 25 And he is not served by human hands, as if he needed anything. Rather, he himself gives everyone life and breath and everything else. 26 From one man he made all the nations, that they should inhabit the whole earth; and he marked out their appointed times in history and the boundaries of their lands. 27 God did this so that they would seek him and perhaps reach out for him and find him, though he is not far from any one of us. 28 ‘For in him we live and move and have our being.’[b] As some of your own poets have said, ‘We are his offspring.’[c]

29 “Therefore since we are God’s offspring, we should not think that the divine being is like gold or silver or stone—an image made by human design and skill. 

God did not just create the world, set everything in motion, and then leave it away; He rules over His creation. We are accountable to the Him who created us; and we should acknowledge Him as the Lord of our life. God is the one who takes the initiative to seek and save the lost; therefore, we need to respond to the call that God continually makes, to be under His rule and the leadership of the Holy Spirit.


JUMATANO TAREHE 16 JUNI 202I   ASUBUHI                       

MATENDO 17:24-29

24 Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;
25 wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.
26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;
27 ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.
28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.
29 Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu.

Mungu baada ya uumbaji, hakuweka kila kitu mahali pake na kisha kuviacha tu; anatawala uumbaji wake wote. Sisi tunawajibika mbele zake yeye aliyetuumba; na tunahitaji kutambua kuwa ndiye Bwana wa maisha yetu. Mungu ndiye aliyechukua hatua ya kutafuta na kuwaokoa waliopotea; hivyo, tunahitaji kuitikia wito wake ambao kila mara ametuita, kuwa chini ya utawala wake na uongozi wa Roho Mtakatifu.