Matangazo ya Usharika tarehe 24 April 2022

MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 24 APRIL, 2022

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI KRISTO AJIFUNUA KWETU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti. 

3. Matoleo ya Tarehe 17/04/2022

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Washarika waadhimisha Pasaka 2022

Usharika wa KKKT Kanisa Kuu Azania Front Cathedral umejumuika na wakristo wote ulimwenguni kusherehekea sikukuu ya Pasaka ya mwaka 2022.

Akizungumza katika ibada ya kwanza iliyofanyika Usharikani hapa, Baba Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dk. Alex Gehaz Malasusa alisema sikukuu ya Pasaka ni muhimu sana katika maisha ya mkristo kwani ni kumbukumbu ya kushinda umauti kwa mwokozi wetu Yesu Kristo.