Date: 
13-04-2022
Reading: 
Waebrania 3:1-6

Juma Takatifu;

Jumatano asubuhi tarehe 13.04.2022

Waebrania 3:1-6

1 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu,

2 aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.

3 Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba.

4 Maana kila nyumba imetengenezwa na mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu.

5 Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye;

6 bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya taraja letu mpaka mwisho.

Hosana ndiye mbarikiwa;

Ajaye kwa jina la Bwana.

Musa alitumwa na Mungu kuongoza watu wake kuelekea nchi ya ahadi. Yesu alikuja kuokoa ulimwengu toka dhambini. Kati yao, Yesu Kristo anakuwa Kuhani Mkuu, maana yeye ni mwokozi wa ulimwengu, tofauti na Musa aliyekuwa kiongozi tu wa msafara. Hivyo Yesu anastahili utukufu kuliko Musa, na mwingine awaye yote.

Kwa ujasiri tunakumbushwa kumpokea huyu Kuhani Mkuu, Yesu Kristo mwana wa Mungu, ambaye kazi yake iliyotukuka ndiyo imetupa wokovu. Musa alikuwa shuhuda tu wa kazi za Mungu, bali Yesu aliifanya kazi ya Mungu, yaani kuokoa ulimwengu. Umempokea moyoni mwako?

Siku njema.