Date: 
22-06-2022
Reading: 
Yohana 17:17-19

Jumatano asubuhi tarehe 22.06.2022

Yohana 17:17-19

17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.
 
18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.
 
19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.

Msigombane njiani;

Sura ya 17 ya Injili ya Yohana huaminika ndiyo sala ndefu iliyoandikwa, aliyosali Yesu. Katika sala hii Yesu aliliombea umoja Kanisa lake. Kwa sehemu, leo asubuhi tunaona Yesu akiliombea Kanisa lake utakaso kwa njia ya neno lake, ili liwe Kanisa moja katika yeye.

Yesu hakutuacha tuishi kwa utengano, bali kwa umoja. Hakuishia kutuelekeza tu, bali kutuombea umoja kwa Baba. Tunakumbushwa kuwa umoja ni tabia ya Mungu (Yoh 17:11) nasi tukialikwa kuwa na umoja kama Mungu wetu alivyo. Umoja utatuweka pamoja ili tusigombane njiani.

Siku njema.