MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 17 AGOSTI, 2025
SIKU YA BWANA YA 9 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA NI
TUENENDE KWA HEKIMA YA MUNGU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 10/08/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 10/08/2025 ni Washarika 641 Sunday School 234,
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Uongozi wa vijana Azania unapenda kuwashukuru vijana wote walioshiriki kwenye mechi ya jumapili iliyopita tarehe 10/8/25 mchezo ulikuwa mzuri na vijana wa Azania walishinda kwa goli 1-0. Zidi ya Tabata , Tunawapongeza vijana kwa ushindi. Leo jumapili watacheza mchezo wa mwisho wa kundi lao na Vijana wa Machimbo saa 10.00 jioni viwanja vya Kenton Mwenge. Washarika mnakaribishwa kwenda kuwashangilia vijana wetu.
8. Tarehe 29/08/2025 Kutakuwa na Mkesha wa maombi ya wanawake na mabinti jimbo la kati utakaofanyika Usharika wa Kariakoo kuanzia saa tatu 3.00 usiku. Wanawake na Mabinti mnaombwa kushiriki mkesha huo wa maombi bila kukosa.
9. Wanawake wa mtaa wetu wa Tabora leo tena wameleta mbogamboga na vitu vingine vya shambani walivyovuna mashambani kwao, vitu hivyo vitauzwa baada ya ibada zote hapo nje. Washarika karibuni kununua mazao fresh kutoka shambani. Wanawake mtaa wetu wa Tabora leo tena wameleta mbogamboga na vitu vingine vya shambani walivyovuna mashambani kwao, vitu hivyo vitauzwa baada ya ibada zote hapo nje. Washarika karibuni kununua mazao fresh kutoka shambani.
10. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 13.09.2025
SAA 6:00 MCHANA
-
Bw.Emanuel Joseaugusto Alexandre na Bi. Sania Martin Kasyanju
KWA MARA YA PILI TUNANGAZA NDOA YA TAREHE 30/08/2025
SAA 9.00 ALASIRI
-
Bw. Stuart Gamaliel Kisyombe na Bi. Paschalina Marijani Msofe
11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mzee Charles Lyimo
- Upanga: Kwa Bw & Bi William Sabaya
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bw & Bi Francis & Happy Mwaitembo
- Kinondoni: Kwa Mama Hilda Lwezaula.
- Mjini kati: Itakuwa hapa Kanisani jumamosi saa moja kamili asubuhi
- Oysterbay/Masaki: Kwa Lightness Moshi
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bw & Bi Jane Matandiko
- Kawe,Mikocheni, Mbezi Beach: Kwa Mama Elisiana Swai
12. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
13. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.