Ijumaa asubuhi tarehe 17.06.2022
Warumi 9:1-8
1 Nasema kweli katika Kristo, sisemi uongo, dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu,
2 ya kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu.
3 Kwa maana ningeweza kuomba mimi mwenyewe niharimishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili;
4 ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake;
5 ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina.
6 Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.
7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa;
8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao.
Mungu mmoja;
Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;
Mtume Paulo anaeleza kuwa kweli ya neno la Mungu haiwezi kubadilika. Ni wale wanaolitii neno la Mungu wanayo nafasi ya kuwa wana wake. Hii ndiyo kweli ambayo Paulo anasema siyo uongo, na katika hili anasema anashuhudiwa na Roho Mtakatifu.
Paulo anaonesha kukomaa katika imani, akisema kuwa neno la Mungu linaishi bila woga. Tutafakari kama nasi tumekomaa kiasi cha kumshuhudia Kristo bila woga, maana huo ndiyo utume wetu.
Siku njema.