Date: 
12-05-2022
Reading: 
Neno la Mungu Leo Hii

Kutoka 16:11-15

--------------------------------------------

11 Bwana akasema na Musa, akinena,
12 Nimeyasikia manung'uniko ya wana wa Israeli; haya sema nao, ukinena, Wakati wa jioni mtakula nyama, na wakati wa asubuhi mtashiba mkate; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
13 Ikawa wakati wa jioni, kware wakakaribia, wakakifunikiza kituo; na wakati wa asubuhi umande ulikuwa juu ya nchi pande zote za kituo.
14 Na ulipoinuka ule umande uliokuwa juu ya nchi, kumbe! Juu ya uso wa bara kitu kidogo kilichoviringana, kidogo kama sakitu juu ya nchi.
15 Wana wa Israeli walipokiona, wakaambiana, Nini hiki? Maana hawakujua ni kitu gani. Musa akawaambia, Ndio mkate ambao Bwana amewapa ninyi, mle.

Maisha mapya ndani ya Yesu;

Kuna wakati Israeli walimlalamimia Mungu kwa kukosa chakula walichopata wakiwa Misri. Walimnung'unikia Musa. Ndiyo tunasoma asubuhi ya leo Mungu akisikia kunung'ujika kwao na kuwapa mikate. 

Bwana aliwasikia Israeli akawapa chakula wakiwa njiani kuelekea nchi ya ahadi. Kumbe nasi tukimuita Bwana hutusikia, akitupa haja zetu. Hii  ni neema yake kwetu. Tunadumuje katika neema hii? Ni Kwa kumwamini, tukimcha na kutenda mema, ili atupe haja zetu na maisha mapya kuelekea uzima wa milele