Date: 
11-05-2022
Reading: 
Neno la Mungu Leo Hii

Marko 8:34-38

----------------------------------------

34 Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate.
35 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.
36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
37 Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?
38 Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.

Maisha mapya ndani ya Yesu;

Yesu anafundisha juu ya kumfuata, kwamba atakaye kumfuata sharti ajitwike msalaba wake amfuate. Hapa alimaanisha kumpelekea yeye (Yesu) dhambi inayozuia kumfuata ili asaidie kuifuta. Yesu anasisitiza kuwa haina maana mtu kufurahia ulimwengu akaikosa mbingu!

Yesu anatufundisha kuwa maisha tunayoishi yana mwisho. Tufahamu kuwa ipo siku tutaiacha dunia hii. Tutakwenda wapi?  Tusiionee haya Injili, ili naye Bwana asituonee haya mwisho wa safari yetu (38).
Mwisho wetu utategemea kama maisha yetu ni mapya katika Kristo Yesu.