Date: 
10-05-2022
Reading: 
Neno la Mungu Leo Hii

Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.

Maisha mapya ndani ya Yesu;

Yesu alikuwa akieleza jinsi ambavyo angekufa na kufufuka. Kabla ya mstari tuliosoma alisema;
Yohana 16:16  Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni; na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona.
Yalikuwa maneno mazito, lakini ilikuwa lazima kuyasemz  ili kuwaandaa wanafunzi wake na kifo chake.

Baada ya kufa alifufuka, alipowatokea walifurahi kama somo la usiku huu linavyoonesha. Kwa kufufuka kwa Yesu tunayo maisha mapya tukijawa furaha ya milele. Jambo la muhimu ni kuhakikisha hii furaha isituondokee, maana yake tusimwache Yesu aliyefufuka kwa ajili yetu.