Date: 
20-01-2023
Reading: 
Mithali 3:34

Ijumaa asubuhi tarehe 20.01.2023

Mithali 3:33

[33]Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, 
Bali huibariki maskani ya mwenye haki.

Nyumba zetu hubarikiwa na Mungu;

Tangu kale hata sasa Mungu huuchukia uovu. Biblia huonesha watu waliofanya uovu na Bwana akawaadhibu, mfano ni Sodoma na Gomora. Pia kumbuka wakati wa Nuhu Mungu alipoangamiza watu kwa mvua ya siku 40 kwa sababu ya uovu. Somo la asubuhi hii linasema kuwa Laana ya Bwana i katika nyumba ya waovu, na Bwana huibariki maskani ya mwenye haki.

Bwana anatuagiza kuacha uovu ili laana isiingie nyumbani mwetu. Tunaweza kuuacha uovu kwa kumpokea Yesu na kuishi kwa kadri ya mapenzi yake. Tukiacha uovu tunakuwa wenye haki, na Mungu hutubariki. Chukua hatua ya Imani kwa kuacha uovu, ili baraka za Mungu ziwe kwenye nyumba zetu.

Ijumaa njema.