Date: 
14-06-2022
Reading: 
Mathayo 28:19-20

Jumanne asubuhi tarehe 14.06.2022

Mathayo 28:19-20

19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
 
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Mungu mmoja;

Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;

Baada ya kufufuka Yesu aliwatokea wale kumi na moja, akawaachia utume wa kuhubiri Injili. Ndilo somo la leo asubuhi, ambapo Yesu anawatuma wanafunzi kuhubiri kote katika utatu Mtakatifu, yeye akiahidi kuwa nao.

Muktadha wa agizo la Yesu katika somo la leo asubuhi hii ni kuhubiri neno la Mungu kwa usahihi. Yaani tumhubiri Mungu wa utatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Hii ndiyo kweli. Siku njema.