Date: 
20-06-2022
Reading: 
Matendo ya Mitume 14:26-28

Jumatatu asubuhi tarehe 20.06.2022

Matendo ya Mitume 14:26-28

26 Na kutoka huko wakaabiri kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza.

27 Hata walipofika wakalikutanisha kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwamba amewafungulia Mataifa mlango wa imani.

28 Wakaketi huko wakati usiokuwa mchache, pamoja na wanafunzi.

Msigombane njiani;

Mtume Paulo akiwa na Barnaba na wengine wanaendelea na utume wao waliopewa na Yesu Kristo. Walifanya kazi kubwa iliyotukuka, na leo asubuhi tunaona wakielekea Antiokia ambapo "walilikutanisha Kanisa" wakiihubiri habari njema ya wokovu. 

Paulo na wenzake wanaliweka Kanisa pamoja kwa kuhubiri habari njema. Injili waliyoihubiri haikumtangaza Kristo tu, bali iliwaunganisha watu. Kwa mahubiri na mafundisho watu waliletwa pamoja. Ni ushuhuda kwetu kukaa pamoja kama Taifa la Mungu. Tusigombane njiani.

Uwe na wiki njema isiyo na kugombana njiani.