Date: 
26-01-2023
Reading: 
Hesabu 27:1-11

Alhamisi asubuhi tarehe 26.01.2023

Hesabu 27:1-11

[1]Wakati huo wakakaribia hao binti za Selofehadi, mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, wa jamaa za Manase mwana wa Yusufu; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya; Mala, na Noa, na Hogla, na Milka, na Tirsa.

[2]Nao wakasimama mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya wakuu, na mkutano wote, mlangoni pa hema ya kukutania, wakasema,

[3]Babaetu alikufa nyikani, naye hakuwamo katika mkutano wa hao waliojikutanisha kinyume cha BWANA katika mkutano wa Kora; lakini akafa katika dhambi zake mwenyewe; naye alikuwa hana wana wa kiume.

[4]Kwa nini basi jina la babaetu kufutwa katika jamaa zake kwa sababu alikuwa hana mwana wa kiume? Tupe sisi urithi pamoja na ndugu zake babaetu.

[5]Basi Musa akaleta neno lao mbele ya BWANA

[6]BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

[7]Hao binti za Selofehadi wananena lililo haki; kweli utawapa milki ya urithi pamoja na ndugu za baba yao; nawe utawapa urithi wa baba yao.

[8]Kisha utanena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Mtu akifa, naye hana mwana wa kiume, ndipo utampa binti yake urithi wake.

[9]Tena ikiwa hana binti, mtawapa nduguze urithi wake.

[10]Na ikiwa hana ndugu, mtawapa ndugu za babaye huo urithi wake.

[11]Tena ikiwa babaye hana ndugu, utampa huyo aliye karibu naye katika jamaa zake huo urithi wake, naye atakuwa nao; na neno hili litakuwa ni amri ya hukumu kwa wana wa Israeli, kama BWANA alivyomwagiza Musa.

Yesu anaondoa ubaguzi;

Binti za Solefohadi walilalamika mbele ya Musa na Makuhani kwamba baada ya baba yao kufa walinyimwa urithi. Kupitia Musa Bwana aliamuru wapewe urithi. Pale ndipo Bwana alitoa maelekezo kuwa ikitokea mtu amekufa bila ya kuwa na mtoto wa kiume, urithi apewe binti yake. Na kama hana binti pia, ndio wapewe ndugu wengine.

Ipo dhana ya usawa katika ugawaji mali katika somo la asubuhi hii. Lakini zaidi ya hapo tupo katika jamii inayowanyima watu haki zao kwa sababu ya jinsia, rangi, kabila, Imani n.k Yesu aliondoa ubaguzi wa namna yoyote alipokufa kwa ajili ya wote. Mgawanyo wa mali na majukumu uzingatie haki katika Kristo Yesu, na siyo ubaguzi.

Siku njema.