AZANIAFRONT DELEGATION VISITS MESSIAH - OCTOBER 2017

WASHARIKA 14 WA AZANIAFRONT WAZURU USHARIKA RAFIKI WA MESSIAH, MARQUETTE, MICHIGAN, MAREKANI OKTOBA 2017

Washarika 14 wa umri mbali mbali na wenye fani mbali mbali walipata nafasi ya kuzuru Usharika rafiki wa Messiah tarehe 5 - 19/10/2017 wakiongozwa na Mch P. Chuwa. Waliweza kushiriki shughuli za ibada za Messiah kwa jumapili 2, shuhuli za kijamii, na kutembelea maeneo ya kuvutia jirani na usharika huo. Pia walitembelea kituo cha kiroho cha Fortune Lake. Wamejifunza mengi katika ziara hiyo ambayo watayatumia katika maisha yao na Usharikani Azania pia.