Date: 
18-05-2022
Reading: 
2Watheselonike 2:13-17

Jumatano asubuhi tarehe 18.05.2022

2 Wathesalonike 2:13-17

13 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;

14 aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.

15 Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.

16 Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,

17 awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema.

Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana;

Mtume Paulo anawakumbusha Wathesalonike kuwa wameitwa na Mungu katika utume wao, hivyo wamshukuru kwa neema hiyo. Anawausia kusimama imara wakiyashika waliyofundishwa toka walipompokea Yesu. 

Sisi nasi tumeitwa na Yesu Kristo, akatutakasa kwa Roho Mtakatifu wake ili tupate kuyatangaza matendo yake. Yeye ndiye aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema. Tudumu katika yeye tukimsifu bila kukoma.

Siku njema.