Date: 
21-01-2023
Reading: 
2Wafalme 4:8-17

Jumamosi asubuhi tarehe 21.01.2023

2 Wafalme 4:8-17

[8]Hata ikawa siku moja, Elisha alikwenda Shunemu; na huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo; naye akamshurutisha aje ale chakula. Ikawa kila alipopita njia ile, huingia kula chakula.

[9]Yule mwanamke akamwambia mumewe, Tazama, mimi naona ya kuwa mtu huyu apitaye kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu.

[10]Nakuomba, tumfanyie chumba kidogo ukutani; na ndani yake tumwekee kitanda, na meza, na kiti, na kinara cha taa; na itakuwa, atujiapo, ataingia humo.

[11]Ikawa siku moja akafika huko, akaingia katika chumba kile akalala.

[12]Akamwambia Gehazi mtumishi wake, Mwite yule Mshunami. Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mbele yake.

[13]Akamwambia, Sema naye sasa, Tazama, wewe umetutunza sana namna hii; utendewe nini basi? Je! Uombewe neno kwa mfalme, au kwa amiri wa jeshi? Yule mwanamke akamjibu, Mimi ninakaa katika watu wangu mwenyewe.

[14]Akasema, Basi, atendewe nini? Gehazi akajibu, Hakika hana mwana, na mumewe ni mzee.

[15]Akamwambia, Kamwite. Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mlangoni.

[16]Akasema, Panapo wakati huu mwakani, utamkumbatia mwana. Akasema, La! Bwana wangu, wewe mtu wa Mungu, usiniambie mimi mjakazi wako uongo.

[17]Yule mwanamke akachukua mimba, akazaa mtoto mume wakati uo huo mwakani, kama Elisha alivyomwambia.

Nyumba zetu hubarikiwa na Mungu;

Elisha alitunzwa nyumbani kwa mwanamke mshunami akiwa katika huduma yake. Baadaye Elisha akamuuliza yule mwanamke kwamba Bwana amtendee nini? Mama akaomba mtoto, na Elisha akamwambia kuwa katika mwaka ujao angepata mtoto. Alipata mtoto, na ukiendelea kusoma mbele kidogo unaona kuwa mtoto yule alikufa. Lakini bado walimfuata Elisha ambaye aliomba kwa jina la Bwana mtoto akafufuka.

Nyumba ya mama mshunami ilijaa baraka za Mungu kuanzia mafuta yaliyolipa deni, kupata mtoto na mtoto aliyekufa kufufuka. 

Kwa kumwendea Elisha wakati ule, nyumba ile ilimtegemea Bwana. 

Ni wito kwa familia zetu kuwa tegemezi kwa Bwana na siyo kwa dunia. Tumfanye Bwana awe tegemeo letu katika nyumba zetu sasa na siku zote.

Siku njema.