Date: 
30-05-2022
Reading: 
2Samweli 22:7-16

Jumatatu asubuhi 30.05.2022

2 Samweli 22:7-16

7 Katika shida yangu nalimwita Bwana, Naam, nikamlalamikia Mungu wangu;

8 Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka, Misingi ya mbinguni ikasuka-suka Na kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu.

9 Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala; Makaa yakawashwa nao.

10 Aliziinamisha mbingu akashuka; Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.

11 Akapanda juu ya kerubi akaruka; Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo.

12 Akafanya giza hema zake za kumzunguka, Makusanyiko ya maji, mawingu makuu ya mbinguni.

13 Toka mwangaza uliokuwa mbele zake Makaa ya moto yakawashwa.

14 Bwana alipiga radi toka mbinguni, Naye Aliye juu akaitoa sauti yake.

15 Akapiga mishale, akawatawanya; Umeme, naye akawatapanya.

16 Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake Bwana, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.

Sikia kuomba kwetu;

Asubuhi hii tunamsoma mtu aliyemuita Bwana na kumlalamikia katika shida yake. Mungu anaonekana wenye ghadhabu hadi misingi ya mbingu kutikisika. Mstari wa 17 unaonesha Mungu akijibu sala ya aliyeomba msaada wake.

Mungu hapendi tukae dhambini, ndiyo maana kila wakati tunakumbushwa kutubu. Tabia yake ni kusamehe. Tunapotubu yeye hutusikia, maana kama alivyotuagiza kuomba, yeye husikia kuomba kwetu.

Nakuombea Mungu asikie kuomba kwako.

Uwe na wiki njema.