Date: 
02-07-2022
Reading: 
Warumi 10:16-21

Jumamosi asubuhi tarehe 02.07.2022

Warumi 10:16-21

16 Lakini si wote walioitii ile habari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, ni nani aliyeziamini habari zetu?

17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

18 Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.

19 Lakini nasema, Je! Waisraeli hawakufahamu? Kwanza Musa anena, Nitawatia wivu kwa watu ambao si taifa, Kwa taifa lisilo na fahamu nitawaghadhibisha.

20 Na Isaya anao ujasiri mwingi, asema, Nalipatikana nao wasionitafuta, Nalidhihirika kwao wasioniulizia.

21 Lakini kwa Israeli asema, Mchana kutwa naliwanyoshea mikono watu wasiotii na wakaidi.

Wito wa kuingia katika ufalme wa Mungu;

Mtume Paulo anaandika juu ya imani kuwa imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo. Paulo anarejea enzi ya manabii, kuwa walihubiri na Sauti yao ilisikika na kuenea kote. Lakini bado wapo waliokuwa wakaidi (21)

Asubuhi hii tunapokea ujumbe wa kuwa na imani, yaani kusikia neno la Mungu na kumwamini Yesu. Tusiwe wakaidi tunaposikia neno la Mungu. Tukisikia, tukaamini, tutaingia katika ufalme wa Mungu.

Jumamosi njema.