Date: 
07-07-2022
Reading: 
Tito 3:12-15

Alhamis asubuhi tarehe 07.07.2022

Tito 3:12-15

12 Wakati nitakapomtuma Artema kwako au Tikiko, jitahidi kuja kwangu huku Nikopoli; kwa maana huku nimekusudia kukaa wakati wa baridi.

13 Zena, yule mwana-sheria, na Apolo, uwasafirishe kwa bidii, wasipungukiwe na cho chote.

14 Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.

15 Watu wote walio pamoja nami wakusalimu. Tusalimie wale watupendao katika imani. Neema na iwe pamoja nanyi nyote.

Kijana na uchumi katika zama za utandawazi;

Mtume Paulo anamwandikia Tito kuwa awafundishe na kuwasihi watu wadumu wakitenda mema wakizaa matunda. Paulo alikuwa akimwambia Tito asiwe mvivu, bali afanye kazi ya Mungu, na kazi hiyo izae matunda yanayoonekana. 

Tunapotafakari nafasi ya kijana katika uchumi na maisha kwa ujumla, kama Paulo anavyomuagiza Tito, sisi sote tunaalikwa kuwa na bidii katika kazi ya Mungu, tuzae matunda. Tusiwe wavivu.

Siku njema.