Date: 
14-02-2017
Reading: 
Romans 9:14-18 (NIV)

TUESDAY 14TH FEBRUARY 2017 MORNING                          

Romans 9:14-18  New International Version (NIV)

14 What then shall we say? Is God unjust? Not at all! 15 For he says to Moses,

“I will have mercy on whom I have mercy,
    and I will have compassion on whom I have compassion.”[a]

16 It does not, therefore, depend on human desire or effort, but on God’s mercy. 17 For Scripture says to Pharaoh: “I raised you up for this very purpose, that I might display my power in you and that my name might be proclaimed in all the earth.”[b] 18 Therefore God has mercy on whom he wants to have mercy, and he hardens whom he wants to harden.

Footnotes:

  1. Romans 9:15 Exodus 33:19
  2. Romans 9:17 Exodus 9:16

Our God is a merciful and loving God who is not willing for any to perish. God draws us to Himself. Let us come to Him in faith and repentance.

JUMANNE TAREHE 14  FEBRUARI 2017 ASUBUHI                      

RUMI 9:14-18

14 Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha! 
15 Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. 
16 Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu. 
17 Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote. 
18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu. 
 

Mungu ni Mungu wa upendo na huruma. Yesu alikufa kwa binadamu wote. Mungu anatuvuta kwa upendo wake ili tumwamini.

Tuje kwa Mungu kwa toba na imani.