Date: 
23-08-2017
Reading: 
Romans 1:28-32 NIV (Warumi 1:20-32)

WEDNESDAY 23RD AUGUST 2017 MORNING                               

Romans 1:28-32  New International Version (NIV)

28 Furthermore, just as they did not think it worthwhile to retain the knowledge of God, so God gave them over to a depraved mind, so that they do what ought not to be done. 29 They have become filled with every kind of wickedness, evil, greed and depravity. They are full of envy, murder, strife, deceit and malice. They are gossips, 30 slanderers, God-haters, insolent, arrogant and boastful; they invent ways of doing evil; they disobey their parents; 31 they have no understanding, no fidelity, no love, no mercy. 32 Although they know God’s righteous decree that those who do such things deserve death, they not only continue to do these very things but also approve of those who practice them.

The Apostle Paul is warning the Christians in Rome about people who refuse to believe the truth. There are those who refuse to obey God’s laws and try to justify their sins. We all have consciences which warn us when we are about to do wrong. However if we repeatedly ignore our conscience and mix with people who also engage in sinful behavior we can become immune and feel that we are OK. May God give us all a sensitivity to and hatred of sin. Let us ask God to examine our hearts and lives and help us to cast out anything which is not pleasing to Him.

JUMATANO TAREHE 23 AGOSTI 2017 ASUBUHI                           

WARUMI 1:28-32

28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. 
29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, 
30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, 
31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; 
32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.

Mtume Paulo alikuwa anaandikia Wakristo kule Rumi kuwaonya kuhusu watu ambao wamezama katika matendo mabaya. Sisi sote tumepewa dhamiri na Mungu ambaye inatuonya tukitaka kutenda dhambi. Lakini watu ambao wanandelea kutenda dhambi na kujichanganya na watu wenye matendo maovu wanakuta kwamba wanatenda dhambi bila aibu. Wengine hata wanajisifu kwa dhambi zao. Mungu atusaidie kuchukia dhambi. Mungu atusaidie kujichunguza mioyo yetu na kuacha yyote yasio safi mbele za Mungu katika mawazo na mwenendo wetu.