Date: 
31-05-2024
Reading: 
1Wakorintho 16:1-4

Ijumaa asubuhi tarehe 31.05.2024

1 Wakorintho 16:1-4

1 Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.

2 Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;

3 nami nitakapofika nitawatuma kwa nyaraka wale mtakaowachagua, wachukue hisani yenu mpaka Yerusalemu.

4 Na kama ikifaa niende na mimi, watasafiri pamoja nami.

Utatu Mtakatifu; Iweni na nia ya Kristo;

Mtume Paulo anarejea wito ambao aliwahi kuutoa huko nyuma kwa ajili ya kwachangia maskini. Ziko sehemu kadhaa, asubuhi hii twaweza kurejea hapa;

Warumi 15:25-26

25 Ila sasa ninakwenda Yerusalemu, nikiwahudumu watakatifu;
26 maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo kwa ajili ya watakatifu huko Yerusalemu walio maskini.

Mtume Paulo anaelekeza kila mtu kuweka akiba, lakini kufanya changizo kwa ajili ya wasiojiweza. Hapa upo ujumbe kwetu kama Kanisa kukaa pamoja kwa upendo tukisaidiana na kushirikiana. Kama Kanisa ni wito wetu kusaidia wasiojiweza. Mimi na wewe tunaitwa kuwa sehemu ya kuimarisha kazi ya diakonia, kwa ajili ya Utukufu wa Mungu. Huo ndiyo umoja tunaoagizwa kuwa nao. Amina.

Ijumaa njema

Heri Buberwa